Proverbs 6:6-11


6 aEwe mvivu, mwendee mchwa;
zitafakari njia zake ukapate hekima!
7Kwa maana yeye hana msimamizi,
wala mwangalizi, au mtawala,
8 blakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi
na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

9 cEwe mvivu, utalala hata lini?
Utaamka lini kutoka usingizi wako?
10 dBado kulala kidogo, kusinzia kidogo,
bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:
11 ehivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi,
na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.
Copyright information for SwhNEN